Rais wa Congo aondoka nchini leo
Uncategorize
Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ( DRC), ameondoka nchini hii leo baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili.
Kiwa hapa nchini katoka ziara yake ya kikazi Rais Tshisekedi pamoja na mambo mengine alipokelewa na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan na kuwa na mazungumzo ya faragha Ikulu, Dar es Salaam.
Viongozi hao pia walishuhudia utiaji saini wa mikataba inayohusu ushirikiano wa mawasiliano kati ya Tanzania na DRC.
Hiyo ilikuwa ni ziara ya kwanza ya Rais Tshisekedi nchini Tanzania tangu serikali ya awamu ya sita ilipoingia madarakani, na ni ziara yake ya pili akiwa Rais wa DRC
Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere uliopo Jijini Dar es Salaam, Rais Tshisekedi ameagwa na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan.

No comments
Post a Comment