Header Ads

Header ADS

Uganda yaweka masheriti 21 kukabiliana na ugonjwa wa Ebola

 

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameweka mashariti 21 ya kuzuia maambuzi ya ugonjwa wa Ebola ya Sudani , mlipuko uliotangazwa nchini humo tarehe 20 Septemba 2022.

Moaka kufikia jana watu 58 wamethibitishwa kuambukizwa Ebola, 19 wamefariki na 20 wamepona wakiwemo Madaktari na wafanyakazi wa sekta ya afya.

Katika hotuba yake kwa taifa usiku wa kuamkia leo masharti hayo aliyoweka ni pamoja na kuweka zuio kuanzia leo Junaoili la watu kutotoka nje katika wilaya za Mubende na Kasanda kuliko bainika mgonjwa wa kwanza.

Nyumba za Ibada zote zimefungwa pamoja na maeneo ya starehehe ikiwemo Baa, kumbi za disko, vibanda vya filamu pamoja na shughuli zote za michezo.

Usafiri wa umma na binafsi yaani mabasi, dalala, magari ya watu binafisi na boda boda kuuanzia leo zimezuiwa kutotembea usiku kuanzia saa moja jioni hadi saa kumi na mbili asubuhi.

Hatua hii ya Rais Museveni inafutiia ombi la chama cha Madaktari nchini humo mwezi jana kupitia kwa rais wao Samuel Oledo waliomba Rais Museveni kuziweka karantini wilaya zilizo na maambukizi.

Hata hivyo mpaka sasa wilaya tano ndizo zilizo na maambukizi lakini zikizoguswa ni mbili kunakotajwa ndiko chimbuko la mlipuko wa sasa.

No comments

Powered by Blogger.