Header Ads

Header ADS

Wadau wa Maendeleo kufanya Mkutano wa pamoja na Serikali

 

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiongoza kikao kati ya wadau wa maendeleo na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango (hawapo pichani), kuhusu maandalizi ya mkutano kati ya Tanzania na wadau wa maendeleo utakaofanyika hivi karibuni.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na  Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, baada ya kikao na Mwenyekiti Mwenza wa Washirika wa Maendeleo nchini, Mhe. Zlatan Milisic (hayupo pichani), kuhusu maandalizi ya mkutano kati ya Tanzania na wadau wa maendeleo utakaofanyika hivi karibuni. Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma.

Mwenyekiti Mwenza wa Washirika wa Maendeleo nchini, Mhe. Zlatan Milisic, akizungumza jambo katika kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kilichojadili kuhusu maandalizi ya mkutano kati ya Serikali na wadau wa maendeleo unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni. Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban na Kamishna wa Idara ya Fedha za nje, Bw. Rished Bade, waakifuatilia majadiliano ya maandalizi ya mkutano kati ya Tanzania na wadau wa maendeleo, utakao fanyika hivi karibuni.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa nne kushoto), Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. David Concar (wa tatu kushoto), na Mwenyekiti Mwenza wa Washirika wa Maendeleo nchini, Mhe. Zlatan Milisic (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa maandalizi ya mkutano kati ya Serikali na wadau wa maendeleo, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amefanya kikao na Mwenyekiti Mwenza wa Washirika wa Maendeleo nchini, Mhe. Zlatan Milisic, kuhusu ushirikiano wa maendeleo na maandalizi ya mkutano kati ya Serikali na washirika hao utakaofanyika hivi karibuni.

Dkt. Nchemba amefanya kikao hicho jijini Dodoma na Mwenyekiti Mwenza wa Washirika wa Maendeleo nchini, Mhe. Zlatan Milisic, ambapo ajenda mbalimbali za mkutano huo ziliangaziwa.

Alisema kuwa miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa katika mkutano huo utakaofanyika hivi karibuni ni pamoja na kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji, ajira kwa vijana, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kilimo.

Ajenda nyingine ni kukuza uchumi, uhifadhi wa chakula, nishati kwa wote, uwezeshaji wa wanawake na utaratibu wa ushirikiano katika masuala ya kifedha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ametoa dira ya kukuza uchumi kwa kuwaleta wawekezaji na kuweka mazingira bora ya uwekezaji na biashara jambo ambalo pia linaendelea kutekelezwa kupitia wadau wa maendeleo”, alieleza Dkt. Nchemba.

Alisema kuwa Serikali  kupitia Wizara ya Fedha na Mipango itaratibu ushiriki wa Wizara nyingine za kisekta kushiriki kikamilifu katika mkutano huo ili kuwa na manufaa makubwa  kwa pande zote mbili.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mwenza wa Washirika wa Maendeleo nchini, Bw. Zlatan Milisic, alisema washirika wa maendeleo wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika majadiliano yanayo hamasisha maendeleo ya wananchi katika kukuza mitaji, ajira na pia uwezeshaji wa wanawake.

Wadau wa maendeleo wameahidi kuendelea kudumisha ushirikiano na Tanzania katika masuala mbalimbali na kushiriki katika ukuzaji wa uchumi kwa manufaa ya pande zote.

No comments

Powered by Blogger.