Header Ads

Header ADS

Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dare s Salam asema hataki Machawa na badala yake awataka Viongozi kuchapa kazi

 Mwenyekiti  wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salam, Khadija Ally, amesema hataki machawa na badala yake anataka viongozi na wanachama wa jumuiya hiyo kuchapa kazi.

Akizungumza leo Desemba 14, 2022 katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam Khadija amesema yeye sio Mwenyekiti wa Chawa ,hivyo anachotaka kuona viongozi na wanachama wa jumuiya hiyo wanafanya kazi kuanzia ngazi ya Kata, kuangalia malenzi ya Watoto, maadili na elimu katika shule zinazomilikiwa na jumuiya hiyo.

“Tufanye kazi zionekane, jamii ifaidike, tuwe viongozi wenye maadili, viongozi tunapaswa kuwa mfano wa kuigwa, hatuwezi kuwa viongozi ambao hatuna maadili,"amesema Mwenyekiti huyo

Ametumia nafasi hiyo kueleza anaandaa mafunzo maalum ya uongozi yenye lengo la kukumbushana misingi ya jumuiya, maadili ya uongozi na malezi.

“Hatuwezi kuwa na kiongozi asiye na maadili, tuwe na uongozi shirikishi sio uongozi wa kimungu, utakachosema ndio hicho hicho .Hutaki ushauri, hutaki kusikia lolote kwa mtu yoyote, hapana! uongozi lazima uwe shirikisho.”

Aidha, katika kikao hicho pia umefanyika uchaguzi mdogo wa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya jumuiya hiyo.Walioshinda nafasi ya Baraza la Mkoa na Kamati ya utekelezaji Wazazi Mkoa ni Omar Ngurangwa, Muhammad Abdulghafur na Busoro Pazi.









No comments

Powered by Blogger.