Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa anapaswa kushtakiwa baada ya mamilioni ya pesa kukutwa shambani kwake
Jopo la watu watatu lililoundwa kuuliza iwapo Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anapaswa kushtakiwa baada ya mamilioni ya pesa kukutwa katika shamba lake litawasilisha mapendekezo yake Bungeni Jumatano Desemba 7, 2022.
Jopo hilo, lililoundwa Septemba 2022, lilitaka kupata ushahidi wowote wa awali wa makosa ya rais mwezi Juni 2022, baada ya kuibiwa kwa takriban dola milioni 4 katika shamba hilo mwaka 2020, na kuibua utata kuhusu jinsi rais bilionea alivyozipata pesa hizo.
Rais Ramaphosa alithibitisha kutokea kwa wizi, na alisema fedha hizo zilitokana na mauzo ya ambapo muda wa kashfa hiyo hauwezi kuwa mbaya zaidi kwani rais amesalia chini ya mwezi mmoja kabla ya mkutano wa uchaguzi utakaoamua iwapo atawania muhula wa pili kwa tiketi ya chama tawala cha African National Congress (ANC) katika uchaguzi wa 2024.
Jaji Mkuu wa zamani na Mwenyekiti wa jopo, Sandile Ngcobo amesema, “Pendekezo la kumburuza rais kabla ya mchakato wa kumuondoa madarakani ni uamuzi mkubwa, hauwezi kufanywa kwa misingi isiyo na msingi, lazima liwe jambo linaloonekana.”
Uchunguzi huo ni tofauti na uchunguzi wa makosa ya jinai ambao polisi wanafanya, na ambao Ramaphosa ameukaribisha huku ripoti hiyo itajadiliwa katika bunge la kitaifa Desemba 6, 2022 na Spika wa Bunge, Nosiviwe Mapisa-Nqakula.
No comments
Post a Comment