Header Ads

Header ADS

Rufaa ya Ongwen yatupiliwa mbali na ICC

 

 Mahakama ya rufaa ya uhalifu wa kimataifa ICC, imetupilia mbali rufaa ya aliyekuwa kamanda wa kundi la waasi la Lords resistance Army LRA, la nchini Uganda Dominic Ongwen, na kuhalilisha huku aliyopewa ya miaka 25 gerezani.

Ong'wen alihukumiwa baada ya kuhifadhi na makosa ya uhalifu wa kivita, na uhalifu dhidi ya binadamu.

Hukumu hiyo ilitolewa karibu miaka miwili baadaye baada ya Ongwen kuhifadhi na hatia katika makosa 61 yaliyokuwa yanamkabidhi, yakiwemo mauaji, unajisi, ndoa za lazima na kusajili Watoto kuwa wapiganaji, kati yam waka 2002 na 2005.

Mawakili wake walikuwa wameasilisha hoja 90 katika rufaa hiyo, kwamba maombi na makosa ya ukweli, kimakakati na wakati wa kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi dhidi yake.

Jopo la majaji watano wakiongozwa na Jaji Luz del Carmen Ibanez Carranza, amesema kwamba mahakama ya rufaa imekataa rufaa hiyo na kuidhinisha hukumu ya miaka 25 kushinda dhidi ya Dominic Ongwen.

Kundi la waasi la LRA linaongozwa na Joseph Kony, ambaye ni miongoni mwa viongozi wakubwa wa waasi wanaosakwa kote duniani.

No comments

Powered by Blogger.