Umoja wa Vyuo Vikuu waandaa Tamasha la Kuinjilisha
Umoja wa vijana kutoka vyuo vikuu mbalimbali kutoka jimbo kuu la Dar es Salaam wameandaa tamasha kubwa lenye lengo la kuinjilisha kwa njia ya mkesha hasa katika kuwaombea vijana, kusali, kuabudu, kumtukuza na kumshukuru Mungu lakini pia kuliombea Taifa kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Padri wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Padri Vitalis Kassembo amesema kuwa Mkesha huo unatarakiwa kuanza leo ijumaa Desemba 16, 2022 na kumalizika Jumamosi Desemba 17, 2022.
Kuhusu lengo lingine la Tamasha hilo Padri Kassembo amesema ni kuwafanya vijana wawe na hofu ya Mungu katika kila jambo wanalolifanya.
“Vijana wanamambo mengi hivyo wanahitaji neema za Mungu,ndiyo maana wameamua kuwashirikisha na vijana wenzao kuja na tamasha hili ambalo litawafanya wawe na hofu ya Mungu “
Naye Mratibu Karesmatiki kutoka kanisa katoliki jimbo kuu Dar es salaam, Ludovick Kawishe alisema Tukio mkesha huo utakua ni wa kipekee sana kwani vijana wanapokutana watajengeana uwezo, na kubadilisha mawazo ambapo watakua na hofu ya kuendelea kumtumikia Mungu lakini .
Kwa upande wake Katibu Maandalizi ya mkesha wa usiku wa sifa, Ronaldo Chota alisema Mkesha huo hauna kiingilio na wamewalenga sana wanafunzi wa vyuo ambao baadhi yao hupenda kujihusisha na makundi yasiyofaa, ambapo tayari wamevifikia vyuo 51.
No comments
Post a Comment