Header Ads

Header ADS

Zoezi la ufunguzi wa lango la handaki la mchepuko wa bwawa la Mwalimu Nyerere kufunguliea 22 Desemba 2022


 Zoezi la Ufunguzi wa lango la handaki la mchepuko wa bwawa la mwalimu nyerere linatarajiwa kufunguliwa rasmi alhamsi tarehe 22 December 2022 ambapo Rais *Samia Suluhu Hassan* anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kushuhudia ufunguzi wa lango hilo la handaki mchepuko(diversion tunnel) ili kuruhusu maji yaanze kujaa katika Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere ambapo viongozi mbali mbali wa serikali, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, pamoja na baadhi ya wananchi watakuwepo, hata hivyo tukio hilo litarushwa mubashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Mradi wa bwawa la Mwalimu nyerere ulianza 2019 hadi sasa tayari umefikia asilimia sabini na nane(78) ya ujenzi na unatarajiwa kuisha June 2024 ukiwa umegharimu trillion 6.5

Hayo yamesemwa leo tarehe 18 December na Waziri wa Nishati January Makamba alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo katika bonde la mto Rufiji mkoani Pwani alipotembelea ili kujionea mwenendo wa ujenzi wa mradi huo.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa shirika la umeme Tanzania (Tanesco) Ndugu *Maharage Chande* amesema kwamba itachukua misimu miwili ya mvua kulijaza bwawa hilo huku akiongeza kwamba litahifadhi lita Bilion 33.2 za maji ambazo zitaweza kuendesha mitambo kwa kipindi cha Mwaka mmoja.

Aidha mradi huo utawasaidia wananchi kwenye mradi wa kilimo chini ya Yam Rufiji, kuondoka mafuriko pamoja nakupata umeme wa uhakika

No comments

Powered by Blogger.