Baraza la mitihani NECTA limesitisha utaratibu wa kutangaza shule bora na mwanafunzi bora wa matokeo ya kidato cha nne
Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania NECTA Athumani Salumu Amasi amesema utaratibu huo wa kutangaza shule bora ulikuwa unazitangazia biashara baadhi ya shule
“Kutangaza shule ya kwanza huenda tulikuwa tunakufanyia Marketing kwa kuitaja tu hiyo shule, shule zipo nyingi zaidi ya elfu 18, sasa unapotaja moja sidhani kama ina tija” amesema Athumani Salumu
Kuhusu kumtangaza mwanafunzi bora wa mtihani huo amesema hakuna tija katika hilo kwani hauwezi kumtangaza mwanafunzi mmoja katika ya wanafunzi wote Tanzania ambao huenda pia mazingira yao ya kusoma yalikuwa tofauti
“Unamtaja mtu kwamba ameongoza katika kundi ambalo pamoja na kwamba wamefanya mtihani huo huo lakini hawakusoma katika mazingira yanayofanana, alafu sasa unampa sifa mtu mmoja” amesema Athumani Salumu
No comments
Post a Comment