Header Ads

Header ADS

Chama Cha ACT Wazalendo Cha shauri Serikali kuja na mpango mkakati maalum



 CHAMA Cha ACT Wazalendo kimeishauri Serikali kuja na mpango mkakati maalum ambaoutasaidia kumaliza au kupunguza kwa kiasi kikubwa deni la ndani ambalo limekuwa kwa asilimia 30 na athari zake zinakwenda moja kwa moja kwa wananchi.

Akizungumza leo Januari 15,2023 Waziri wa Fedha na Mipango wa Chama cha ACT Wazalendo Emmanuel Mvula amesema wameipitia ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania( BoT) na inaonesha kukua kwa kiwango kikubwa kwa deni la Taifa likiwemo deni la ndani.

Amesema deni la ndani ni hatari na kwamba limeongezeka kutoka Sh 18.6 mpaka 26.6, ni fedha nyingi huku akifafanua deni la ndani linatokana na Serikali kukopa kukopa benki za ndani, mifuko ya hifadhi ya jamiii, bima na watu binafsi kwa kupatia hatifungani.

"Serikali imekopa asilimia 27 ya deni ndani la ndani na kwenye deni hilo asilimia 28 imekopwa kutoka Taasisi za fedha, asilimia 18 zinatoka bima na asilimia nyingine kwa watu binafsi.Kwa kipindi cha miaka 20 kumekuwa na ukuaji wa hili deni.Mwaka 2005 deni la nje lilikuwa dola bilioni nane sawa na trilioni tisa na deni la ndani lilikuwa Sh.Trilioni 1.7

"Mwaka 2015 wakati Rais Mstaafu Jakaya Kikwete anatoka madarakani deni la nje lilikuwa dola bilioni 15.4 wakati deni la ndani likiwa Sh.trilioni 7.9. Hiyo ilikuwa miaka 10 ya Kikwete na alipoingia Rais Dk.John Magufuli hadi kufika Machi deni la nje lilikuwa dola bilioni 24 na deni la ndani Sh.trilioni 16.1.Wakati wa Rais Samia Suluhu Hassan naingia hadi kufikia Novemba mwaka 2022 deni la nje limefikia Dola bilioni 27.5 na deni la ndani Sh.trilioni 26,"amesema Mvula.

Amesema kukua kwa deni la Taifa hasa deni la ndani athari zake zinakwenda kwa moja kwa moja kwa wananchi huku akieleza deni la ndani halitakiwi kuzidi asilimia 20 na kama nchi tuko asilimia 10 zaidi."Athari yake nyingine ifahamike tunatumia fedha nyingi kulipa deni.

"Makusanyo yetu ya ndani yanatumika kulipa deni .Tunatumia bilioni 900 kwa mwezi kulipa deni la Taifa. Kila mwezi tunalipa na kati ya hizo Sh.bilioni 600 zinatumika kulipa deni la ndani na bilioni 300 zinalipa deni la nje.Kwa hiyo hii inafanya Serikali kutumia fedha nyingi kulipa madeni kuliko kufanya maendeleo.

"Tukisema madeni haya yanatokana na Serikali kukopa katika taasisi za ndani, watu binafsi na kampuni za bima deni linapotakiwa kulipwa Serikali inabidi iingie tena kukopa fedha kwa ajili ya kulipa, hivyo Serikali inakopa zaidi na inaingia kwenye soko la ndani kukopa na inapokopa inaleta ushindani."

Amessema ili kupata fedha za kulipa deni ndio unaona kumekuwepo na utitiri wa kodi,athari nyingine ni kwenda kukopa kwenye mifuko ya hifadhi ya mifuko ya jamii na hivyo inakwenda kuathiri mifuko hiyo na wastaafu kutolipwa pensheni zao kwa wakati.

"Madeni hayo yanasababisha mzigo mkubwa kwa wananchi .Kutokana na maelezo hayo ACT Wazalendo tunatoa pendekezo ili kuondoa deni

hili Serikali ije na mkakati maalum wa kumaliza deni hilo kwenye bajeti ya mwaka huu na kwa kuwa tunakwenda kwenye maandalizi ya bajeti basi tunaitaka Serikali ije na mkakati wa kumaliza deni ,"amesema Mvula.


No comments

Powered by Blogger.