Header Ads

Header ADS

Mhe. George Simbachawene awapongeza Wajumbe Wa Kamati Ya Kudumu Ya Bunge Sheria

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amewapongeza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Sheria Ndogo kwa kazi kubwa ya kuchambua sheria Ndogo zilizowasilishwa katika mkutano wa tisa wa Bunge.

Waziri ameyasema hayo leo tarehe 20/01/2023 katika ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo inaisaidia Serikali ili iwezee kufanya mambo kwa kuzingatia haki na sheria.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene (kushoto) akizungumza baada ya kupokea Jedwali la Uchambuzi la Sheria Ndogo.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene leo asubuhi pokea Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu Sheria Ndogo Mhe. Kilumbe Shabani Ng’enda Bungeni Mjini Dodoma.Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu Sheria Ndogo Mhe. Kilumbe Shabani Ng’enda (kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhi Jedwali la Uchambuzi la Sheria Ndogo.


No comments

Powered by Blogger.