Mwili wa Mtanzania Nemes Tarimo ambaye alifariki October 24,2022 akiwa vitani nchini Ukraine baada ya kujiunga na Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group umewasili katika Uwanja wa Ndege wa J.K Nyerere Dar es salaam asubuhi ya leo Ijumaa January 27,2023 ambapo utaagwa na kusafirishwa hadi Mbeya upande wa Mama yake kwa ajili ya maziko.

Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali ya Tanzania iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax mapema Wiki hii, Nemes alifariki akiwa vitani nchini Ukraine baada ya kujiunga na Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group akiwa anatumikia sehemu ya kifungo chake cha miaka saba alichofungwa kwa makosa ya kihalifu.

Waziri Tax alinukuliwa akisema “Tarimo akiwa gerezani alipewa nafasi ya kujiunga na kikundi cha kijeshi cha Wagner kwa ahadi ya kulipwa fedha lakini kwa ahadi ya kuachiwa huru mara baada ya vita na umauti ulimkuta October 24,2022 na Wizara ikawasiliana na Serikali ya Urusi ili kukabidhiwa mwili”

“Nemes Tarimo alikwenda nchini Urusi mwaka 2020 kwa masomo ya shahada ya uzamili katika fani ya biashara , March 2022 alihukumiwa kifungo cha miaka saba kwa vitendo vya uhalifu