NECTA yatangaza matokeo kidato cha nne 87.79% wafaulu
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) Athumani Amasi, ametangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika Novemba 14 hadi Desemba 1, 2022, Tanzania Bara na Visiwani huku likiwafutia wanafunzi 333 kwa udanganyifu.
Ameyasema hayo wakato akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 29, 2023, amesema kati ya watahiniwa hao mmoja ni wa maarifa (QT) na 332 watahiniwa wa shule.
“Baraza limefuta matokeo ya watahiniwa 333 kwa kufanya udanganyifu, kati yao mmoja ni mtahiniwa wa maarifa na 332 ni wa shule,” amesema
Ametaja watahiniwa wengine waliofutiwa matokeo ni wanne ambao wameandika matusi katika mitihani yao.
Amasi amesema vituo vitatu vimefungiwa kufanya mitihani baada ya kuthibitika kupanga na kufanya udanganyifu ambapoa amevitaja vituo hivyo ni Andrew Faza Memorial cha Kinondoni Dar es Salaam, Cornelius cha Kinondoni na Mnemonic Academy cha Halmashauri ya Mjini Magharibi visiwani Zanzibar.
Aidha amesema kati ya watahiniwa 520,558 wenye matokeo 456,975 sawa na asilimia 87.79 wamefaulu kwa kupata madaraja ya kwanza hadi la nne.
Amasi, ameeleza ufaulu huo umeongezeka kwa asilimia 0.49 kutoka wa mwaka jana ambapo watahiniwa 422,388 sawa na asilimia 87.30 walifaulu.
No comments
Post a Comment