Waziri Mkuu wa Italia yupo Libya kwa mazungumzo
Televisheni ya taifa nchini Libya imesema Waziri Mkuu huyo wa Italia alipokelewa na Abdelhamid Dbeibah ambaye anaongoza serikali ya umoja wa kitaifa yenye makao yake mjini Tripoli ambayo inazozaniwa na utawala hasimu wa mashariki mwa nchi hiyo
Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni aliwasili Jumamosi katika mji mkuu wa Libya wa Tripoli kwa mazungumzo kuhusu nishati pamoja na suala zito la uhamiaji vyombo vya habari vya serikali ya Libya vimesema.
Ziara ya Meloni ambayo ni ya pili katika nchi ya Afrika Kaskazini wiki hii ni ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Ulaya nchini Libya ambayo ilikumbwa na vita tangu ziara ya mtangulizi wake Mario Draghi mwezi Aprili 2021.
Televisheni ya taifa imesema Waziri Mkuu huyo wa Italia alipokelewa na Abdelhamid Dbeibah ambaye anaongoza serikali ya umoja wa kitaifa yenye makao yake mjini Tripoli ambayo inazozaniwa na utawala hasimu wa mashariki mwa nchi hiyo.
Libya na utawala wa zamani wa kikoloni Italia ni washirika wakuu wa biashara, hasa katika nishati, ambako kampuni kubwa ya Italia, ya Eni ina jukumu kubwa katika kusimamia akiba kubwa sana ya mafuta barani Afrika.
Meloni alifuatana na mkuu wa kampuni ya Eni, Claudio Descalzi, ambaye anatarajiwa kutia saini makubaliano na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Libya kuendeleza maeneo mawili ya gesi kwenye pwani ya Libya.
No comments
Post a Comment