Mahakama moja nchini Kenya imewahukumu maafisa watatu wa polisi na mtoa habari wao kifungo cha miongo kadhaa jela siku ya Ijumaa kwa mauaji ya wakili wa haki za binadamu Willie Kimani na watu wengine wawili mwaka 2016.


Mahakama moja nchini Kenya imewahukumu maafisa watatu wa polisi na mtoa habari wao kifungo cha miongo kadhaa jela siku ya Ijumaa kwa tuhuma za mauaji ya wakili wa haki za binadamu Willie Kimani na watu wengine wawili mwaka 2016.


Kesi hiyo ilizua hasira nchini Kenya, ambako polisi wanakabiliwa mara kwa mara na shutuma za ukatili na mauaji holela, lakini mara nyingi hawashtakiwi.


Kimani, mteja wake Josephat Mwendwa na dereva wao, Joseph Muiruri, waliuawa muda mfupi baada ya kuwasilisha malalamiko ya ukatili wa polisi, yakidai kuwa Mwendwa alipigwa risasi na kujeruhiwa na polisi.


Miili yao baadaye iliopolewa kutoka kwenye mto uliopo nje ya mji mkuu Nairobi. Washtakiwa hao wanne walikutwa na hatia ya mauaji mwaka jana


Mshtakiwa wa kwanza Frederick Leliman, alihukumiwa


kifo. Hata hivyo, Kenya haijamnyonga mtu yeyote tangu mwaka 1987, kawaida adhabu za vifo hubadilishwa kuwa kifungo cha maisha jela. Maafisa wengine wawili wa polisi, Stephen Cheburet na Sylvia Wanjiku, na mtoa habari wao Peter Ngugi, walihukumiwa vifungo vya miaka 20 hadi 30 jela.

Jaji huyo, Jessie Lessit, alielezea mauaji hayo kuwa “yalipangwa na kutekelezwa vizuri".

Msemaji wa polisi alisema polisi watatoa taarifa baadaye.

Polisi wanasema wanachukua hatua dhidi ya afisa yeyote anayetuhumiwa kwa ukatili, wakati mamlaka huru ya Kusimamia Polisi (IPOA), chombo kilichoundwa kuchunguza kesi za ukatili wa polisi, inachunguza kesi kama hizi na kupendekeza mashtaka yafunguliwe.


Mamlaka hiyo ya uangalizi ilisema hukumu hiyo imetoa afueni kwa jamaa, marafiki na wafanyakazi wenza wa waathirika.


Wakati alipofariki, Kimani alikuwa akifanya kazi na

ofisi ya International Justice Mission, kikundi cha kimataifa cha haki za kisheria ambacho husaidia kuchunguza na kuweka kumbukumbu za mauaji na ukatili unaofanywa na polisi