Marekani inashuku kuwa vitu vitatu ambavyo ilivindungua havikuwa tishio
Vitu hivyo vinaweza "kuhusishwa na taasisi za kibiashara au utafiti na kwa hivyo sio hatari," msemaji John Kirby alisema.
Maafisa wa Marekani na Canada bado hawajapata au mabaki ya ndege hizo tatu zilizoanguka.
Beijing hapo awali ilishutumu Marekani kwa "kwa kuchukua hatua ya haraka kupindukia’
China imekanusha kuwa moja ya puto zake, ambayo iliharibiwa na ndege ya kivita ya Marekani mapema mwezi huu karibu na Carolina Kusini, ilikuwa ikitumika kwa ujasusi, ikisema kuwa tu kilikuwa chombo cha anga cha kuangalia hali ya hewa ambacho kilipotea kutoka kwa mkondo wake.
Katika mkutano wa kila siku na wanahabari siku ya Jumanne, Bw Kirby alisema itakuwa vigumu kubaini madhumuni au asili ya vitu vingine vitatu vilivyoharibiwa katika maeneo ya Alaska, Canada na Michigan hadi vifusi vipatikane na kuchambuliwa.
"Hatujaona dalili yoyote au kitu chochote kinachoashiria wazo kwamba vitu hivi vitatu vilikuwa sehemu ya mpango wa kijasusi wa PRC's [Jamhuri ya Watu wa Uchina]," Baraza la Usalama la Kitaifa la White House liliwaambia waandishi wa habari.
No comments
Post a Comment