Ndege iliyoanguka Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga sio Ajali ya Kweli
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita @mboni_mhita amesema taarifa za ajali ya ndege iliyoripotiwa kutokea Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga sio ajali ya kweli bali ni majaribio ya kupima utayari wa kwelkuokoa pindi ajali za ndege zinapotokea ambapo kiuhalisia
hakuna vifo vilivyojitokeza na majeruhi.
Amesema zoezi hilo limeratibiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania na kwamba hufanyika kila baada ya miaka miwili na leo ilikuwa ni zamu ya Kiwanja cha Ndege cha Kahama.
“Tulipokea taarifa ya ajali ya ndege tukafika eneo la tukio tukaja kutambua ni zoezi la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kujipima utayari wa kuokoa, walifanya hilo zoezi kwa usiri mkubwa sana kwasababu wote tulifika hapa, navishukuru Vyombo vyote ambavyo vipo Kahama kwa utayari hata kama walikuwa kwenye utayari imenisaidia kujua Vyombo vyetu vipo na utayari, nimefika eneo la tukio nikaambiwa ni zoezi la kujipima”
No comments
Post a Comment