Header Ads

Header ADS

Serikali kuanzisha mfuko wa Mazingira



Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis amesema Serikali inatarajia kuanzisha Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira.

Akijibu swali la Mbunge wa Donge, Mohammed Jumah Soud bungeni jijini Dodoma hii leo Februari 8, 2023, Khamis amesema lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo, ni kusaidia katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Amesema, kutokana na kupitishwa kwa Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021, Serikali kwa sasa inafanya mapitio ya Sheria ya Mazingira, Sura ya 191 ikiwemo taratibu za kuanzisha Mfuko huo.

Aidha ameongeza kuwa, pamoja na kuwepo kwa changamoto ya uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini, Serikali imeendelea kutenga fedha za ndani kwa ajili ya shughuli za mabadiliko ya tabianchi.
Akiendelea kujibu swali hilo naibu waziri alifafanua kuwa Serikali inaendelea kunufaika na Mifuko ya kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

“Serikali inatambua umuhimu wa kuwepo kwa vyanzo vya fedha vya uhakika ili kuimarisha jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa lengo ili zisaidie wananchi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,” amesema.

No comments

Powered by Blogger.