Header Ads

Header ADS

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe limewataka wazazi na walezi kuhakikisha usalama wa watoto wao katika kipindi hiki cha sikikuu

 

Jeshi la Polisi mkoani Njombe imewataka wazazi na walezi katika kipindi hiki cha sikukuu kujihakikishia usalama wa watoto wao pindi wanapoenda katika viunga mbalimbali kwani kwa sasa kumekuwa na unyanyasaji wa kingono kwa watoto na hasa wakiume na kupelekea watoto hao kuharibikiwa maumbile yao.

Kamanda wa Polisi mkoani wa Njombe Hamis Issah amesema watoto watakapotoka matembezini wazazi ama walezi wahakikishe wanawakagua ili kuhakikisha kuwa wapo salama.

"Sasa hivi kumekuwa na mfumuko wa unyanyasaji unaofanywa na watu wazima ama watoto wenyewe kwa wenyewe ambapo hujenga mahusiano ya jinsia moja kitu ambacho ni kinyume cha maadili"amesema Kamanda Issah

Kuhusu tukio la wanafunzi kadhaa katika moja ya shule ya sekondari mjini Njombe kutajwa kusimamishwa masomo kwa kukutwa na makosa mbali mbali ikiwemo mapenzi ya jinsia moja (Ushoga) amesema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

"Kuna taharuki kwenye mashule ya Sekondari vijana wamejihusisha na mapenzi ya jinsia moja lakini sahizi upelelezi unaendelea itakapokuwa tayari tutaeleza nini kimejiri,na nani amehusika"alisema Kamanda Issah

Aidha amesema jeshi hilo tayari limeimarisha ulinzi katika kipindi hiki cha sikukuu huku akiwataka madereva wa magari mbalimbali kuendesha magari yao kwa uangalifu bila uvunjifu wowote wa sheria ikiwemo kutokutumia kilevi kupilitiza.

No comments

Powered by Blogger.