Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likijadili suala la Palestina
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limepinga Jumatatu usiku mswada wa azimio ulowasilishwa na Rashia unaolaani ghasia zinazoendelea Mashariki ya Kati.
Baadhi ya wajumbe walikataa kunga mkono hoja ya kuilani Hamas pekee yake kwa kufanya shambulio la kushtukiza dhidi ya Israel lililosababisha vifo vya watu 1 400.
Baraza lilishindwa kupitisha mswada wa azimio. wakati Israel ikijitayarisha kufanya shambulio la nchi kavu baada ya mashambulio makubwa ya anga ya mabomu ambayo maafisa wanasema yamesababisha vifo vya karibu watu 2 750.
Ni mataifa manne pekee yaliyounga mkono pendekezo la Rashia, mataifa mengine manne yaliungana na Marekani kupinga na mataifa sita hayajaunga mkono upande wowote.
Wanadiplomasia kwenye Umoja wa Mataifa wanasema pendekezo jingine ambalo limetayarishwa na Brazil ambalo linatumia lugha ya kulaani kundi hilo la wanamgambo wa kislamu linaonekana litapata uungaji mkono zaidi na linatazamiwa kuwasilishwa kupigiwa kura baadae Jumanne .
No comments
Post a Comment