Chama cha ACT WAZALENDO chafanya uchaguzi wa viongozi wa jimbo la Makambako mkoani Njombe
Chama cha ACT Wazalendo kimefanya uchaguzi wa jimbo la makambako katika ngazi mbalimbali za Viongozi ambao umefanyika katika ukumbi wa Malifimbo Mjini Makambako , umehusisha viongozi katika ngazi za vijana,ngome ya wanawake,ngome ya wazee,na viongozi wa jimbo kama mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi na katibu wake.
Akizungumza baada ya uchaguzi mjumbe wa halmashauri kuu ambaye pia ni mgeni rasmi Chiku Afla Abwao , amesema kuwa anashukuru wanachama wote "nashukuru wanachama wote waliofika katika uchaguzi huu na katika uchaguzi kuna kushinda na kushindwa kwa tulichokifanya ni kuangalia nani anafaa kuwa kiongozi na kama umeshindwa katika uchaguzi usijione hufai kuwa kiongozi na kila mtu anatakiwa ndani ya Act Wazalendo pia tunahitaji watanzania wote wawe Act wazalendo pia nawashukuru viongozi waliomaliza mda wao kwa wale ambao wameshindwa wasione mwisho wa Act wazalendo katika maendeleo tuliyoyapata ni pamoja na kushinda katika balaza la mawaziri na sasa kule zanzibar tuna makamu wa Rais ametoka kwenye chama chetu tunajivunia Act Wazalendo"
Aidha,amesema wakipambana kwa pamoja watashinda katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2025 pia amesema wanahitaji nguvu moja ili kushinda uchaguzi ujao,ametoa shukrani kwa viongozi waliopita kwa kufanya kazi nzuri mbaka kufikia leo hii hakika wamejituma na wamefanikisha Act wazalendo tumekuwa wakuigwa katika jamii kupitia viongozi wetu wapya tutazidi kusimamia haki ya kila mwananchi na tuna ahidi kuto waangusha hata mara moja.
Viongozi waliokuwa wakiachia madaraka ya ngazi zao wamesema wanahitaji vijana waajiriwe maana kwa sasa vijana wengi hawana ajira vilevile wamesema katika chama chao hakuna kurudi nyuma na watafuata njia za viongozi wao wakuu kama Zitto Kabwe na wengineo.
Pia,malengo yao ni kuhakikisha wanachama wote wanakuwa waaminifu,na wanakuwa makini ili watavyochagua wenyeviti wa mtaa na vitongoji wawe wagombea wengi katika kila ngazi.
Vilevile,mwenyekiti wa Act wazalendo ndugu Ally Mhagama amesema"amefurahi kupokea wanachama wengine ambao wametoka katika vyama tofauti tofauti pia amewaomba viongozi waliochaguliwa wakawe sauti ya kutatua migogoro hiyo ndiyo kazi ya Act wazalendo.
Kwa upande wake katibu wa Act wazalendo mkoa wa njombe,Stanley Exaudy Mbembati ambaye pia ni naibu waziri kivuli wa jeshi la kujenga taifa"kama ilivyo desturi ya chama chetu cha Act wazalendo tumeendeleza demokrasia wagombea na wajumbe wamejitokeza kwa wingi na tunapenda kuona vijana wakijitokeza kwa wingi na wito wangu wanachama waendelee kupigania haki".
Wakizungumza na machweo media baadhi ya wanachama ambao ni Danido Ngalema amesema anafurahi uchaguzi umekuwa mzuri na wa haki pia ametoa rai kwa vijana wengine wajiunge na Act wazalendo kwa watapata mafanikio mengi wakiwa ndani ya chama.
Mwanachama mwingine ni Bi Richards Kinyamagoha amesema ''uchaguzi nimeupenda kwa sababu viongozi waliopita ni wenye uwezo wa kutatua changamoto zetu na nawashauri wanawake walioshinda wachukue mawazo ya wananchi wapeleke katika ngazi husika.
Hata hivyo,wagombea walioshinda ni,
1.Oscar Mugoba -Mwenyekiti kamati ya uongozi wa jimbo la makambako
2.Joseph Malinga-Katibu kamati ya uongozi wa jimbo la makambako
3.Georad Mbata- kiongozi ngome ya vijana
4.Festo Jay Ngalema -kiongozi ngome ya vijana
5.Vicky Kinyamagoha -mwenyekiti ngome ya wanawake
6.Lestuta Brown-katibu ngome ya wanawake
7.Angle Nyafunga-katibu muenezi
8.Jenifer Lazaro-katibu wa mipango
9.Michael Charles Nyasemwa- katibu habari na uenezi
10.Abdukarim Sanga-mtunza hazina
................Mwandishi...........
..............Biesha Mgomela, Makambako.
No comments
Post a Comment