Header Ads

Header ADS

Simba yashauliwa kutoa taarifa TAKUKURU kama imebaini vitendo vya Rushwa katika mchezo wake dhidi ya Yanga Sc.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene ameiomba klabu ya Simba kama imebaini vitendo vya rushwa katika mchezo wake dhidi ya Yanga SC uliochezwa November 5, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam itoe taarifa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) Manispaa ya Temeke ili hatua ziweze kuchukuliwa.

    Hayo yamesemwa  na Simbachawene , leo November 8, 2023 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Nyongeza la Mbunge wa Makete, Festo Sanga aliyetaka kujua mkakati wa Serikali kupambana na rushwa michezoni akitolewa mfano baadhi ya Wachezaji wa Simba kusimamishwa kwa madai ya kuwepo kwa viashiria vya rushwa katika mchezo huo.

Awali akijibu Swali hilo Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma amesema Wizara kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekua ikipinga vitendo vya rushwa michezoni ambapo kwa kushirikiana na TAKUKURU wamekua wakitoa Elimu kuhusu suala hilo na kwamba tayari wameaanzisha Kampeni inayoitwa “Kataa upangaji wa matokeo, linda hadhi ya mpira wa miguu” ambayo inaendelea kuleta matokeo mazuri pia kushirikiana na Wadau wengine wa michezo vikiwemo vilabu husika kupinga vitendo hivyo. 

No comments

Powered by Blogger.