Header Ads

Header ADS

Rc Mndeme aweka jiwe la msingi Halmashauri ya Msalala

 

Na Biesha Mgomela

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme ameweka jiwe la msingi kwenye jengo jipya la ofisi za halmashauri ya Msalala wilayani Kahama ujenzi uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 4.  

Zoezi hilo la uwekaji wa jiwe la msingi limefayika leo Desemba 12, 2023 kwenye jengo jipya la ofisi za halmashauri ya Msalala lililopo kata ya Segese ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga ikiongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Christina Mndeme kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya wilaya ya Kahama.

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amezitaka halmashauri ya Ushetu, Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa kuiga mfano na hatua hizo za ujenzi kwa ajili ya ofisi za watumishi na kuipongeza halmashauri ya Msalala kwa hatua za ukamilishaji wa jengo hilo la ofisi za halmashauri.

“Moja ya malengo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ni kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi, ni kweli mlikuwa mkifanya kazi katika mazingira magumu lakini kwa sasa historia imeandikwa ndani ya halmashauri hii hongereni sana, kukamilisha jengo hili ni hatua moja hatua inayofuata ni utoaji wa huduma bora kwa wananchi, tuboreshe zaidi utoaji wa huduma bora kwa wananchi, lakini kupitia jengo hili mipango mizuri yenye manufaa ndani ya halmashauri hii ipangwe kwenye jengo hili na kuleta mabadiliko chanya kwa wakazi wa Msalala”, amesema RC Mndeme.

“Na kupitia jengo hili natoa maelekezo kwa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, Ushetu na wilaya ya Shinyanga waige hatua hizi, ninyi mmekuwa mfano wa halmashauri zingine kwa sababu bado wanasuasua na hasa Shinyanga DC na Manispaa, lakini niwapongeze kwa kutumia samani za ndani zilizotengenezwa ndani ya mkoa huu hatua hii ni uungaji mkono wa shughuli zinazofanywa na wajasiriamali wazawa”, ameongeza RC Mndeme.

Muonekano wa Nje wa jengo la ofisi za halmashauri ya Msalala.

Zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi likiendelea.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Mibako Mabubu ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo la ofisi kwa ajili ya watumishi na kuongeza motisha kwa watumishi wa halmashauri hiyo.

Aidha kamati hiyo iliyoongozwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme imetembelea kwenye miradi mbalimbali ikiwemo kutembelea na kukagua kituo cha afya Bugarama, ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari ya wasichana ya Bulyanhulu uliogharimu shilingi milioni 851, mradi wa shule ya msingi na sekondari Kabale pamoja na kutembelea mradi wa usambazaji umeme vijijini uliopo kijiji cha Bumva kata ya Segese ambapo mpaka sasa vijiji 16 kati ya 68 vimefikiwa na huduma ya umeme.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akiweka jiwe la msingi kwenye jengo la ofisi za halmashauri ya Msalala.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akikagua jengo la ofisi za halmashauri ya Msalala.


Muonekano wa nje wa jengo la ofisi za halmashauri ya Msalala.



Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Kahama Thomas Myonga akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa usambazaji umeme kijiji cha Bumvu kata ya Segese.


Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa usambazaji umeme kijiji cha Bumvu kata ya Segese.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (KUSHOTO) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Kahama Thomas Myonga.


Mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Mibako Mabubu akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Kahama Thomas Myonga.



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza akiwa kwenye kituo cha afya Bugarama.

Ujenzi wa jengo la kituo cha afya Bugarama.


Majengo ya Shule ya sekondari ya wasichana Bulyanhulu.





 

No comments

Powered by Blogger.