Header Ads

Header ADS

Waathirika wa Mafuriko Hanang wapewa msaada wa Sh.milioni 100 na misaada mingine ya kibinadamu

  

 Pichani ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Amsons Gruop Bhoke Rioba(kulia) akikabidhi hundi ya Sh.milioni 100 kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama (wa pili kushoto)kwa ajili ya mfuko wa maafa kusaidia waathirika wa mafuriko ya matope yaliyotokea Hanang mkoani Manyara. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Dk. Mollel.

Kampuni ya Amsons Group kupitia kampuni zake za Camel Oil na Camel Cement zimekabidhi kiasi cha Sh.milioni 100 kwa Serikali kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko ya matope yaliyotokea Hanang mkoani Manyara.

Aidha, Kampuni ya Camel Oil imetoa misaada mbalimbali kama magodoro, maji na mablanketi kwa ajili ya waathirika hao na hiyo ni sehemu ya kampuni kurejesha tabasamu kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo yaliyosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi ya milioni 100 pamoja na mahitaji hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama ameishukuru kampuni hiyo kwa kutoa fedha na msaada huo kwa ajili ya waathirika wa mafuriko hayo.

Baada ya kupokea fedha pichani ni viongozi wakipokea misaada mingine kutoka Amsons Group 

“Tumepokea Sh.milioni 100 kutoka Camel Cement lakini na vitu vingine kutoka Camel Oil na tunaomba kwa niaba ya Serikali mtupelekee salamu kwa menejiment tunashukuru.

pia,waziri Jenista Mhagama amesema"Bado tunahitaji misaada kwaajili ya ndugu zetu ili kurejesha maisha yao ya kawaida maana kuna waathirika wamepoteza makazi na biashara zao.

wakati akikabidhi misaada hiyo Meneja Masoko na Uhusiano wa Umma wa Amsons Group, Bhoke Rioba amesema Camel Cement imeweka fedha kwenye akaunti ya maafa ya Serikali kiasi cha Sh.milioni 100, magodoro 100 pamoja na mashuka 100.

Amesema kutoa kwao fedha na msaada huo ni muendelezo wa kampuni hizo kwenye kampeni yake ya kurudisha tabasamu kwa jamii ya Tanzania na kuhakikisha kila mwananchi aliyepata janga hilo anapata faraja katika kipindi hiki kigumu wanachokipitia wakazi wa Hanang.

  Na.................Biesha Mgomela..............

                              Manyara


No comments

Powered by Blogger.