LOWASSA AENDELEA NA ZIARA YAKE YA KAMPENI MKOANI DODOMA
Chopa ya
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, ikitua kwenye Uwanja wa Taifa
wa Gairo Mkoani Morogoro, ikiwa ni sehemu wa muendelezo wa ziara zake za
Kampeni anazoendelea, kwenye maeneo mbali mbali hapa nchini. Mh.
Lowassa leo amefanya Mikutano yake hiyo katika Majimbo ya Gairo,Kibakwe,
Mpwapwa na Kibaigwa Mkoani Dodoma.
Meneja wa Kampeni, John Mrema akisisitiza jambo kwa wananchi wa Mji wa Gairo.
Wakazi wa
Gairo, wakifatilia kwa Makini sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa.
Akiwasalimia wananchi wa Gairo.
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimsikiliza Mgombea Ubunge wa Ukawa
kupitia CHADEMA wa Jimbo la Gairo, Salum Mpanda, wakati akimuelezea
changamoto zinazowakabili wananchi wa Jimbo hilo, katika Mkutano wa
Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Gairo Mkoani Morogoro, leo
Septemba 10, 2015. Kulia ni Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye.
Mgombea Ubunge wa Ukawa kupitia CHADEMA wa Jimbo la Gairo, Salum Mpanda, akiwahutubia wananchi wake.
"Pipozzzzzzzzz........Pawaaaaa......."
Waziri
Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye, akiwaonyesha wananchi wa Jimbo la
Gairo, Mkoani Morogoro, Kiberiti chenye picha ya Mgobea Ubunge wa CCM wa
Jimbo hilo, na kuwataka wasirubunike kirahisi kwa kupewa kitu cha namna
hiyo, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Gairo Mkoani Morogoro, leo
Septemba 10, 2015.
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Gairo
Mkoani Morogoro, wakati wa Mkutano wa Kampeni unaoambatana na kunadi
sera za chama chake, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Gairo Mkoani
Morogoro, leo Septemba 10, 2015.
Vijana wa
Mji wa Gairo wakionyesha kadi za kupiga kura wakati Mgombea Urais wa
Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia.
Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwanadi baadi ya Wagombea UKAWA wa
nafasi ya Udiwani kutoka Kata mbali mbali za Jimbo la Gairo, Mkoani
Morogogo leo Septemba 10, 2015.
No comments
Post a Comment