Chadema kukusanya Bilion 13.9 kwa mwaka kupitia kadi mpya za wanachama zitakazoanzakutolewa mwakani
Chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema kimetangaza kuwa ifikapo januari mwakani kitaanza kutumia kadi mpya za uanachama za kielaktroniki zitakazo kiwezesha kukusanya sh 13.9 Bilioni kwa mwaka na kupunguza utegemezi wa ruzuku ya serikali .
Msimamo huo ulitangazwa jana na Mwenyekiti chama hicho Freemani Mbowe wakati wa mkutano wa ndani ya chama uliofanyika Mkoani Morogoro .
Tofauti na Mbowe viongozi wengine wa chama hicho walioko mikoani ni Edward Lowassa , alioko Dodoma,Frederick Sumaye ,ambaye yupo Singida.
Mbowe alisema mfumo huu utasaidia pia kudhibiti baadhi ya viongozi wasio waaminifu wanaotumia mwanya wa kuuza kadi na kushindwa kuwasilishwa fedha kwenye hazina ya chama.
Alisema kwa mfumo huo mpya kama chadema itakuwa na wastani wa wanachama 100000katika wilaya moja na kila mwanachama kulipa ada ya sh 1000/=kwa mwaka ,maana yake wilaya moja itaingiza sh100 milioni.
No comments
Post a Comment