Umoja na ushindi ndio chanzo cha mafanikio
Hayo yamesemwa na Mke wa Rais wa Zanzibar akizungumza wakati wa mkutano wa Umoja wa wanawake wawakilishi na wabunge wa chama cha mapinduzi [CCM] Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwema Shein ameeleza kuwa umoja na mshikamano ndio njia pekee ya kujiletea maendeleo endelevu katika jamii .
Mama Shein ameyasema hayo kwenye ukumbi wa Ikulu ndogo migombani wakati alipofanya mazungumzo na viongozi wanaounda Umoja wa Wake wa viongozi kwa upande wa Zanzibar ,Wakiwemo Wake wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge pamoja na viongozi wa viti maalum wa Chama cha Mapinduzi [CCM].
Katika maelezo yake Mama Shein akiwa ndiye mlezi wa umoja huo aliwakaribisha wake wa viongozi wa Majimbo yote ya Unguja katika umoja huo na kueleza kuwa mafanikio makubwa yamepatikana ndani ya umoja huo kutokana na ushirikiano uliopo.
No comments
Post a Comment