Header Ads

Header ADS

RC-Shinyanga aongoza kampeni ya kupinga ukatili kwa watoto wa kike

Akizungumza katika siku 16 za kupinga ukatili wa mtoto wa kike mkuu wa Mkoa wa Shinyanga bi-Zainab Telaki ,Ameiongoza kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa huo katika ziara ya kutoa elimu ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika maeneo ya vijijini ambako ndiko vitendo hivi vimeshamili.
       Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  amesema kampeni hiyo anayoifanya kijiji kwa kijiji,mtaa kwa mtaa,na baadaye nyumba hadi nyumba imelenga kuelimisha jamii juu ya athari zinazotokana na ukatili wa watoto wa jinsia ya kike huku akiwaasa wazazi kuacha tamaa ya mali kwa kupokea mahari ya ng"ombe na kuwaoza watoto wa kike wakiwa na umri mdogo hali ambayo imekuwa ikiwakosesha nafasi ya kujiendeleza kielimu.
          Katika hatua nyingine bi-Zainab Teleki amezungumzia umhimu wa kuwaelimisha watoto bila kujali jinsia zao huku baadhi ya wakazi wa mkoa huo wakieleza chanzo cha kushamiri kwa vitendo vya ukatili kwa watoto wa kike.
          Hata hivyo wakati kampeni hiyo ikiendelea idadi ya wanaume wanaohudhuria imeonekana kuwa ndogo huku wanawake wakijitokeza kwa wingi hali inayoashiria bado kuna mfumo dume unatawala katika maisha ya wakazi wa vijijini mkoani Shinyanga.

No comments

Powered by Blogger.