Serikali yaondoa bungeni Mswada wa sheria Madaktari wa meno na wataalamu wa afya shirikishi wa mwaka2016
Akitangaza agizo hilo bungeni Naibu Sipika Dk . Tulia Ackson alisema serikali imeamua kuondoa muswada huo kwa sasa.
Hilo ni agizo la serikali "Alisema Dk Tulia wakati akiahirisha bunge leo asubuhi. Akisungumza na waandishi wa habari ,Naibu Waziri wa afya na maendeleo ya jamii ,na jinsia ,wazee na watoto Dk Hamisi Kigwangala alisema serikali imeuondoa muswada huo kutokana na wadau wa sekta ya afya kutoridhika kwamba hawajatendewa haki .
Alisema japo wadau hao waganga wazaidizi wa meno walishirikishwa katika kutoa maoni kwenye kamati ya kudumu ya bunge ya huduma ya maendeleo ya jamii inaonekana hawajaridhika kutokana na kitendo cha kutoingizwa rasimi kwenye jina la muswada huo kitendoambacho wanaona ni kama dalili za kuondolewa kazini kama ungepitishwa .
Alisema hakuna anayekataa kwamba hao ni wataalamu mhimu katika sekta ya afya isipokuwa hawawezi kutambuliwa kama madaktari kutokana na ukweli kwamba mtu anatambuliwa kuwa daktari kama ana shahada ya kwanza na siyo chini ya hapo.
Aliongeza kuwakumekuwa na tafsiri kwamba wataondolewa kazini au watazuiwa kutoa huduma ya afya ukweli ni kwamba kutoandikwa kwenye jina la muswada hakumaanishwi kwamba wataondolewa kazini na wataendelea kutoa huduma kama wanaotoa huduma nyingine,wenye cheti ,Diploma ,Shahada ya kwanza ya uzamivu na uzamili.
Kada hiyo haifutwi kwani ni kada yenye watoa huduma wengi zaidi ya13000 ni mhimu katika kutoa huduma hasa ya upasuaji wa kina mama wakati wa kujifungua na wanazidi idadi ya madaktari ambao ni takribani 3000na wao ni waajiliwa serikalini"Alisema

No comments
Post a Comment