Header Ads

Header ADS

BUNGE MASWALI NA MAJIBU

    Warizi Mkuu  Kassim Mjaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni  mjini Dodoma februari 2,2017
               






















                                                                                                   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni  Freemani Mbowe wakati alipouliza swali katika kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu  bungeni Mjini Dodoma  februari 2,2017
             
             























Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Raisa Dkt John  John Magufuli hajawahi kutangaza au kutoa kauli ya kufutwa kwa Vyama vya Upinzani nchini .
            Ametoa kauli hiyo leo[februari2,2017] Bungeni Mjini Dodoma  wakati akijibu swali la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ,Mheshimiwa Freeman Mbowe katika kipindi cha maswali kwa waziri mkuu.
            Katika swali la Mheshimiwa Mbowe alisema ,alisema Rais Dkt Magufuli alinukuliwa akisema atahakikisha anafuta Vyama vya Upinzani na ifikapo 2020 hakuna upinzani nchini.
           Pia Mheshimiwa Mbowe alitakakujua nini kauli  ya serikali kuhusu kunyimwa dhamana kwa Mbunge  wa Arusha Mjini mheshimiwa Godbless Lema  ambaye anashikiliwa kwa muda wa miezi mitatu.
        Mbali na Mheshimiwa Lema ,Pia kiongozi huyo alitaka kujua kuhusiana na kufungwa  kwa Mbunge wa Kilombero Mheshimiwa Peter  Lijualikali pamoja na Madiwani sita wa chama hicho ambao wamefungwa na viongozi wengine 2015 wanakabiliwa na kesi mbalimbali..
        Kwanza nataka nikanushe kwamba mheshimiwa Rais hajawahikutangaza kuvivuta vyama vya upinzani .Pia watanzania wote wanajua nchi hii inaongozwa kwa sheria ,kanuni na taratibu ,'' Amesema Waziri Mkuu.
         Waziri mkuu ameongeza kuwa tunajua katika kuendesha nchi tunaendesha kwa miimili unaoweza kuingilia mhimili mwingine .
          Pia watanzania wote wanajua kwamba jambo lolote ambalo lipo mahakamani haliwezi kuzungushw katika mahali pengine popote hivyo siwezi kutumia nafasi hii kuzungumzia mambo yote yanayoendelea chini ya sheria na yaliyo mahakamani ';Alisema Waziri.
       Wakati huohuo waziri amewahakikishia watanzania kuwa swala la upungufu wa sukari kwa kushirikiana na wenye viwanda litapungua.
        Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbnge wa Mvomero Mheshimiwa Suleiman Sadiq aliyetakakujua hali ya sukari ilivyonchini kwa sasa na hatua gani zinachukuliwa na serikali ilikunusuru uhaba wa sukari  nchini.

No comments

Powered by Blogger.