Header Ads

Header ADS

Taarifa kutoka BASATA kuhusu kufungiwa kwa wimbo wa Nay wa Mitego

Baraza la sanaa la Taifa [BASATA ] limeufungia rasimi kutumika kwa namna yoyote ile wimbo WAPO ulioimbwa na msanii wa bongofleva Ney wa Mitego.













     Kwa mjibu wa BASATA kifungu namba nne 4 [L] cha sheria ya BASATA Namba 23 ya mwaka 1984  baraza limepewa jukumu la kusimamia kazi za sanaa na mamlaka za kisheria kuhakikisha yote yanafanyika katika tasinia ya sanaa ya nchi taifa na wasanii katika hali zizizo kuwa salaama.
     Katika kutekeleza majukumu haya Baraza linahakikisha maadili  miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwani au wanapobuni kazi zozote za sanaa .
     Wakati huohuo BASATA linawakumbusha wasanii na wadau wote wa kazi za sanaa nchini kuzingatia ubunifu wa haliya juu kufanyakazi za sanaa ili kufikisha jumbe mbalimbali za kuburudisha,kuelimisha,na kuonya.
     Kadhalika baraza linawaonya wote wanaotumia kazi zilizopigwa marufuku .Ikumbukwe kuwa kutumia kazi zilizopigwa marufuku niukiukwaji wa sheria za nchi ambao hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

No comments

Powered by Blogger.