Header Ads

Header ADS

Urusi;Waandamana kupinga matumizi mabaya ya madaraka.

              Maelfu ya raia wamekusanyika katika maeneo tofauti nchini urusi wakiandamana kile wanachodai matumizi mabaya ya fedha za umma.
     Mkusanyiko mkubwa upo katika mji wa Moscow ambapo shinikizo ni kumtaka waziri mkuu wa urusi Dmitry Medvedev kujiuzulu.
       Wanaharakati wamesema hadi sasa watu 800 wanashikiliwa na polisi.Maandamano haya yanatajwa kuwa ni makubwa zaidi ya yale yaliyowahi kutokea urusi kwa miaka mingi ambapo  wanadai kuwa waziri mkuu wao Dmitry Medvedev amekuwa akitumia fedha za umma kakika mambo yake binafsi kwa kujenga majumba ya kifahari,kununua boti za kifahari,mashamba ya mvinyo na jumba la kufugia bata.





















  Marekani imeilaumu urusi kwa hatua yake ya kuwashikilia mamia ya waandamanaji kwa madai kuwa wanavunja haki dhidi ya maandamano ya amani kwa mujibu wa haki za binadamu.

No comments

Powered by Blogger.