Header Ads

Header ADS

Waziri mkuu alivyofika mwenyewe mgodini Buzwagi kukagua mchanga wa dhahabu

     Waziri mkuu Kassim Majaliwa amefanya ziara kwenye mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama  mkoani Shinyanga na kuchukua sampuli za mchanga katika makontena mbalimbali kwa lengo la kwenda kuyapima kwa wataalamu wa madini ili kubaini kiasi cha madini kilichomo.




      Waziri mkuu amesema wanataka kuona mchanga unaosafirishwa na mwekezaji huyo una kiasi gani cha dhahabu pia serikali inataka kufahamu kama kodi inayolipwa ni sahihi
      Waziri mkuu amechukua sampuli za mchanga kwa lengo la kuondoa mashaka juu ya kinachosafirishwa.Sampuli hizo amezichukua kwenye makontena yaliyofungwa kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi.
      ''Tumeamua kuchukua sampuli za mchanga ambao mwekezaji anasema wanaupeleka nje nchi kwa ajili ya kwenda  kutenganisha madini ya dhahabu na shaba.Hata hivyo nimemuhoji kwa nini mitambo hiyo isiletwe nchini ili kila kitu kifanyike hapahapa".

No comments

Powered by Blogger.