Majani yenye sumu Ngorongoro yanaua wanyama kuliko hata magonjwa-Waziri Makamba
Waziri wa nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais ,Mazingira na Muungano January Makamba ametembelea mikoa mbalimbali Tanzania katika muendelezo wa ziara yake ya mazingira iliyoanza Machi 13,2017.
Moja kati ya sehemu alizotembelea Waziri Makamba ni Ngorongoro Crater ambako alijionea namna bonde hilo maarufu lilivyokuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuota kwa majani yenye sumu ambayo yanahatarisha maisha ya viumbe wanaoishi eneo hilo.
''Ngorongor Crater ni moja ya mbuga kubwa na nzuri duniani,lakini kuna jambo la kusikitisha kuhusu mbuga hii.Hivi karibuni kuna majani yenye sumu ambayo yameota sehemu kubwa ya mbuga hii,na majani haya yamekuwa yakihatarisha maisha ya wanyama hasa wanaokula majani''-January Makamba.
No comments
Post a Comment