Aliyekuwa Mgombea Uraisi 2015 Mheshimiwa Edward Luwassa asemakuwa wanaosemakuwa mimi narudi ccm ,wanaota ndoto na hatarudi kamwe
Luwassa ,ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu ni ni mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Chadema, Amesema ameona kwenye mitandao ya kijamii kuna mtu anasema kuwa anatakakurudi CCM,jambo ambalo amelikana na kusema niupotoshwaji mkubwa na hategemei kurudi kwenye Chama cha CCM ,Pia amekaliliwa akisema kuwa siwezi kurudi ccm hayo ni maneno ya kipuuzi na ndoto za mchana .
Waziri ,huyo mstaafu ameyasema hayo akiwa ameambatana na Mbunge wa Arumeru mh.Joshua Nassarri , Mbunge wa Simanjiro mh. James Milya na baadhi ya viongozi wa chama wa kanda ya kaskazini ili kumnadi mgombea udiwani wa kata Makiba` ,Bi. Joyce Ruther .
Luwassa ,amesema kuwa anaiomba Serikali kupitia chama cha Mapinduzi CCM , iache haraka kutuongoza kwa ukabili Taifa letu halikujengwa kwa misingi hiyo ,Akichambua mfumo mzima wa uongozi serikalini amethibitisha hilo .
Pia ameendelea kusema kuwa hatuwezi kugombana na kuchukiana kwa sababu ya kuhama vyama na wala tusikubali kubaguliwa , hivyo sisi ni Watanzania kwanza lakini binafsi bado naamini mabadiliko ya kweli yatatoka nje ya ccm ,Alisema mh: Luwassa,
No comments
Post a Comment