Waziri wa Maji na umwagiliaji mhandisi Isack Kamwelwa aongoza kikao cha wadau wa kujadili mradi wa maji katika Halmashauri ya Simiyu
Mhandisi Isack Kamwelwa amesema tayari tathimini ya mazingira imekamilika na kazi ya upembuzi yakinifu ipo katika hatua za mwisho na zabuni imepangwa kutangazwa mwezi january 2018 baada ya kukamilika kwa zabuni ya ujenzi wa mradi unao kadiliwa kuchukua muda wa miezi 24 . Serikali kupitia ofisi ya makamu wa Rais na Mazingira iliwasilisha ombi la fedha kwa mfuko wa globla climate fund [GCF] ili kutekeleza mradi wa maji katika Halmashauri zilizopo Mkoa wa Simiyu unao julikana kama Simiyu climate Resilience water supply project .
Kwa mjibu wa Waziri wa Maji na umwagiliaji mradi huu umepangwa kufanyika kwa awamu mbili katika Wilaya tano za Mkoa wa Simiyu ambazo ni Busega ,Barihadi ,Itilima ,Maswa na Miatu .Katika awamu ya kwanza mradi utatekelezwa katika Wilaya za` Buseka ,Itilima na Barihadi , kwa kiasi cha EURO Milioni140.7 Ambazo sawa na takribani shiling bilioni 375.4 zimetengwa kwa ajili ya ukamilishaji wa mradi huo.
Fedha za kuanzia mradi wa kwanza zitachangiwa na Serikali ya Tanzania na washirika wa maendeleo ambao ni GCF na Serikali ya Ujerumani. GCF ,watachangia EURO Milioni 102 ,Serikali ya Ujermani watachangia EURO Milion 25.6 na Serikali itachangia EURO Milioni 13.1 na wananchi kupitia nguvu zao watachangia EURO Milioni 1.5 matumizi ya fedha za GCF na Serikali ya Ujerumani yatasimamiwa na Benki ya Maendeleo ya Ujermani [Kfw].
Lengo kuu la mradi huu ni kuboresha afya na kuongeza uzalishaji wa maji ili kuinua hali ya maisha ya wananchi walioathirika na mabadiliko ya tabia ya nchi katika maeneo husika ya mradi.
No comments
Post a Comment