Uvamizi wa Kikabili Nchini Sudani Kusini wauwa watu 50.
Watu 50 ,wameripotiwa kuuwawa katika mapigano ya kikabila Mashariki mwa Nchi ya Sudani kusini .Huu ni mpango wa kikabila wa hivi karibuni katika nchi hiyo uanoendelea kukabiliwa na mapigano ya mara kwa mara tangu mwaka 2013 .
Waziri wa mambo ya ndani Dut Achuek , amethibitisha kutokea kwa mapigano hayo katika Jimbo la Jonglei , Watu waliouawa ni wanawake 23 na wanaume 19 .Richa ya mauaji hayo makazi yao yaliteketezwa na moto.
Kwa mjibu wa habari kabila la Murle lilivamia kabila la Dinka katika vijiji wanavyoishi na kuanza kuwashambulia kabla ya kuwaangamiza . Makabila yote mawili yanajishughulisha na ufugaji yamekuwayakipigana kwa muda mrefu kutokana na mzozo wa wifu wa mifugo.Ifahamike kuwa mauaji mabaya yalitokea mnamo mwaka 2012 kati ya makabila ya Nuer na Murle na kusababisha watu3000 kuuawa.
No comments
Post a Comment