Header Ads

Header ADS

Maazimisho ya Siku ya ukimwi yafanyika kimkoa katika Mji wa Makambako Mkoa wa Njombe katika viwanja vya Polisi .






































              Katika maazimisho ya siku ya ukimwi yaliyo fanyika kimkoa wa Njombe katika Viwanja vya Polisi  vya Mji mdogo wa Makambako ambaoyo kaulimbiu ya mwaka huu ni changia mfuko wa Ukimwi ili kuokoa maisha, Tanzania bila ukimwi inawezekana.                                                                           Serikali kupitia maazimisho hayo imesema kuwa inatumia jitihada kubwa ya kutoa elimu  ya upimaji wa VVU na utoaji wa elimu kuhusu matumizi sahihi ya dawa za ARV .Hayo yametolewa na mratibu shughuli za ukimwi katika Halmashauri ya Mji wa Makambako ,Dokta ,Magreth Mtasi.
            Dk, Magreth amesemakuwa ukimwi ni tabia isipokuwa maambukizi ya virusi  vya ukimwi yanatokana na tabia au ni huruka ya mtu binafusi Serikali kupitia kitengo cha afya changamoto wanayokumbana nayo ni ile changamoto ya kibinadamu akitolea mfano matumizi sahihi ya kondomu pamoja na matumizi ya dawa. Pia serikali imesema kuwa kiwango cha maabukizi ya ukimwi Mkoani Njombe ni asilimia kumi na nne 14%.





































          Magreth,amesemakuwa ilikupunguza maambukizi ya ukimwi 14% Serikali inakusudia kusambasa kondomu na kutoa elimu ya  matumizi sahihi kwa kuna baadhi ya watu wanaoamini kuwa kutumia kondomu kunamadhara kitu ambacho Dokta magreth amekikanusha hakuna madhara kwa mtu yoyote yanampata kutokana na matumizi ya kondomu kwa sababu kuna kondomu za kike japo kondomu za kike upatikanaji ni mchache sana.






































   Miji mdogo wa Makambako  ni Mji wa kibiashara na kuna mwingiliano mkubwa sana wa watu na ukilinganisha kuwa kuna stasheni ,pamoja na paking ya magari makubwa hivyo ndo maana inachangia kuwepo na msongamano mkubwa wa watu na maambikizi ya VVU kuongezeka.
       Ikiwa wananchi wamejitokeza kwa wingi kupima kwa iari ,wamefurahia kwa kitendo ambacho serikali imetoa elimu ya matumizi sahihi ya kondomu pamoja na matumizi ya dawa za ARV.

                 













           

No comments

Powered by Blogger.