Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dare s Saalam ,aliyesambasa nyufa za Hostel za majengo ya chuo cha UDSM ,aachiwa huru na polisi.
Kumbusho Dawson , Ambaye ni Mbunge wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dare s Saalam , ameachiwa baada ya kuhojiwa na polisi kwa kitendo cha makosa ya mtandao. Kwa mjibu wa ripoti iliyotufikia hivi punde Kumbusho alipelekwa kituo kikuu cha Polisi akitokea Oysterbay, aliko kwenda kulipoti asubuhi baada ya kuachiwa jana usiku kwa dhamana .
Wakili Alex Masaba , amesema Polisi wamemuachia baada ya mahojiano na wanaendelea na upelelezi hivyo wakimwitaji watamwita .
Wakili huyo amesema mteja wake amekamatwa kwa kosa la kusambasa picha zinazo onyesha nyufa kwenye jengo la bweni la chuo hicho .hata hivyo yeye anaamini kilichofanyika si jinai . Masaba , ameendelea kusema kuwa kosa la kusambasa picha zilizo pigwa si jinai kitendo alichokifanya anabidi apongezwe ,alisema.
No comments
Post a Comment