Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, ameagiza kamati ya haki maadili na madaraka ya Bunge kukutana ili kujadili kauli yake ilinayodhalilisha Bunge kama chombo cha kutunga sheria .
Christopher Ole Sendeka ,ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe ,anadaiwa kusambaza sauti kwenye mitandao ya kijamii za kukashifu Bunge kama ni chombo cha kutunga sheria . Sauti hizo zikiwa zimeandikwa kwa lugha ya kimasai ,kiswahili na kiingereza .
Kwa mjibu wa Ofisi ya Bunge imeelezwa kuwa Mkuu huyo wa Mkoa anatakiwa kuitwa mbele ya kamati ya haki ,maadili na madaraka ya Bunge na kuhojiwa.
Ole Sendeka ,ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Simanjiro Mkoa wa Manyara kuanzia mwaka 2005 hadi 2015 kabla ya kuangushwa na James Ole Milya katika uchaguzi mkuu wa 2015.Baada ya hapo aliteuliwa kuwa msemaji mkuu wa chama cha mapinduzi[ CCM] kabla ya kuteuliwa na Rais Jonh Pombe Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
No comments
Post a Comment