Mahakama kuu Nchini Kenya yaamua Uhuru Kenyatta kuwa Raisi wa Kenya
Mahakama ya Juu Nchini Kenya imetoa ufafanuzi kuwa Rais ,Uhuru Kenyatta alichaguliwa kihalali katika zoezi la uchaguzi wa marudio wa Uraisi lilo fanyika 26 october 2017 .Kwa mjibu wa Tume ya Uchaguzi Kinyatta alipata asilimia 98 ya kura katika uchaguzi ulio susiwa na muungano wa Vyama vya upinzani .
kwa mjibu wa taarifa kutoka Mahakama ya Juu nchini humo Majaji sita waliokuwa wana`sikiliza kesi hiyo ya kupinga ushindi wa Bwana Kenyatta wamesema Uhuru Kenyatta alichaguliwa kwa mjibu wa sheria za nchi hiyo .
Kulingana na maelezo ya Tume Huru ya Uchaguzi na mipaka Nchini humo ,IEBC ,waliojitokeza kupiga kura walikuwa chini ya asilimia 39 ya Wakenya milioni 19.6 waliojiandikisha .
Mgombea kupitia muungano wa Vyama vya Upinzani Raila Odinga , ambaye alijitoa kwenye uchaguzi wa marudio aliwashawishi wafuasi wake kususia uchaguzi huo na waandamanaji waliwazuia maafisa wa Tume ya Uchaguzi kufungua vituo vya kupigia kura katika ngome za upinzani.
Kwa mjibu ya Mahaka.ma hiyo walalamikaji watatu waliwasilisha maombi katika mahakama na yote yalitupiliwa mbali.
No comments
Post a Comment