Header Ads

Header ADS

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freemani Mbowe ameitaka serikali kubadili uamuzi wa kuzuia mikutano na shughuli nyine za kisiasa kwa kuwa Tanzania ilisha kubali na kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa kwa mjibu wa sheria .




















                      Mbowe, akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa kumnadi mgombea Udiwani katika kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa ,amesema serikali iliyopo madarakani imechaguliwa  kwa mjibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  hivyo inapaswa kuheshimu sheria pamoja na katiba  ikiwemo sheria namba 5 iliyorejesha mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 kabla ya hapo awali kufutwa  mwaka 1965.
        Naye Mchungaji Msingwa ambaye ndiye Mbunge wa Jimbo hilo la Iringa Mjini amewataka wananchi wa Kata ya Kitwiru kuchagua mgombea wa Chadema  ili aweze kuongeza nguvu kwenye Baraza la Madiwani linaloongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema , ambalo limefanya Manispaa ya Iringa kuwa mfano wa kuigwa katika Halmashauri zilizopo inchini .
      Kwa upande wake Mgombea  udiwani kupitia Chadema , Bahati Chengula amewataka wananchi kumwamini kama walipo mwamini awali  na kumchagua kuwa mwenyekiti wa Mtaa , kazi ambayo ameifanya kwa uadilifu  na kujituma kwa lengo la kusukuma  gurudumu la maendeleo.

No comments

Powered by Blogger.