Taasisi ya kupambana na Rushwa Mkoani Kilimanjaro [Takukuru] imemkamata Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi.
Kamanda wa Takukuru wa Mkoa wa Kilimanjaro Holle Makungu alisema kuwa Daktari Deogratiasi Urio , alikamatwa novemba 15 ,2017Baada ya Taasisi hiyo kupokea malalamiko kutoka kwa ndugu wa mgonjwa kwa mjibu wa kamanda wa Takukuru ,Urio anadaiwa kupokea rushwa ya sh,150,000/=Kutoka kwa ndugu wa mgonjwa aliyekuwa anatakakufanyiwa upasuaji katika Hospitali hiyo.
Daktari huyo alikamatiwa katika mji mdogo wa Himo akiwa kwenye baa moja maarufu iitwayo Mombasa High way baada ya kuwekewa mtego na makachero wetu, alisema kamanda wa Takukuru.
Mgonjwa alikuwa anahitaji kufanyiwa upasuaji wa uvimbe katika kizazi tangu octoba 2017, baada ya kufanyiwa vipimo katika Hospitali hiyo na kugundulika kuwa ana uvimbe.
Bwana Makungu, ametoa rai kwa wauguzi wa Hospitali ya Mawenzi na kwingineko Mkoani kilimanjaro wazingatie viapo ili Hospitali ziwe mfano wa kuingwa katika utoaji wa huduma .
No comments
Post a Comment