Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, inatarajia kuanza kusikiliza ushahidi wa kesi ya kumtukana Rais John Pombe Magufuli.
Hlima Mdee ,ambaye ni Mbnge wa Jimbo la Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Anadaiwa kumtolea lugha za matusi Rais Jonh Pombe Magufuli ,ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kuanza kusikiliza ushahidi wa kesi hiyo Desemba 7/2017.
Wakili wa Serikali Keornad Challo ,amemwambia Hakimu mkazi Mkuu Victoria Nongwa kuwa kesi imeitishwa kwa kuanza kusikilizwa lakini shahidi walie nae anasafari .
Kwa mjibu wa Hakimu Nongwa ,ameahirisha kesi hiyo mpaka Desemba 7,mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikiliza.Mbunge huyo aliposomewa maelezo ya awali inadaiwa July 3,mwaka huu , akiwa makao makuu ya Chadema alitoa lugha za matusi dhidi ya Rais Magufuli.Iliyokaliliwa kuwa Rais anaongeah ovyo hovyo anabidi afungwe breki'
July 4 mwaka huu alikamatwa na polisi maeneo ya Kibangu kisha kupelekwa maeneo ya ZCO ,ambako alihojiwa na kukili kutoa maneno hayo.
No comments
Post a Comment