Rais wa Zimbabwe Robert Mgabe ,amfukuza kazi Makamo wa Rais
Robert Mgabe ,ambaye ndiye Rais wa Zimbabwe amemfuta kazi Makamo wa Rais wa Nchi hiyo ambaye wakati fulani alionekana kama ndiye atakayemridhi kuwa Rais
Kufukuzwa kazi kwa Makamo wa Rais Emmerson Mnangagwa ambaye anaumri wa miaka 75 ,kunaweza kufungua njia kwa Mke wa Mgabe Grace kuwania kiti hicho ambaye alishatangaza nia yake toka miaka mitatu iliyopita .
Kwa mjibu wa Serikali ya Zimbabwe ilishatangaza toka jumatatu kuwa Makamo huyo wa Rais ameshafukushwa kazi mara moja na kuelezwa na Waziri wa Habari Simon Kaya Moyo alipo zungumza na VOA kwamba nikutokana na kuwa alionesha tabia za kukoza uzalendo na uaminifu hasa kwa Rais ..
No comments
Post a Comment