Header Ads

Header ADS

Mgabe akabiliwa na kesi ya shutuma ya ufujwaji bilioni 15 za ushuru uliotokana na almasi

      Rais wa  zamani wa Zimbabwe  Robert  Mugabe anakabiliwa na tuhuma za ufujwaji wa  dola  bilion  15  za ushuru uliotokana na uuzaji wa almasi.Hata hivyo bunge nchini humo limesema baada ya kumsubiri Raisi huyo wa zamani kwa zaidi ya nusu saa  na kukosa kufika mbele ya kamati ya madini na pasipokutoataarifa kwa mwenyekiti wake . Temba Mliswa alisema kuwa uvumilifu wa bunge ulikuwa umefika mwisho.                                                                                                   














             Msilwa  ,alisema kuwa katika barua tunayo muandikia  ambayo ni ya mwisho tunamkumbusha  kuwa tutakuwatunamuita kufika mbele ya kamati hii na tunategemea kwamba haitatubidi  kuchukua hatua ya kumlazimisha Rais huyo wa zamani kufika mbele yetu. Tunatumai kuwa barua hii ya mwisho  itakuwa kitu ambacho atafurahia .Iwapo hatafika mbele ya kamati hii  atakuwa amedharau bunge na kua athali kadhaa za kufanya hivyo .Alisema  Msilwa ambaye ndiye mwenyekiti wa tume.
         Ikumbukwe  kuwa hii ni mara ya pili  kwa Raisi huyo wa zamani wa Zimbabwe mwenye umri wa miaka 94 , kukosa kufika mbele ya kamati hiyo ili kujibu tuhuma zinazo mkabili.

No comments

Powered by Blogger.