Mwenge wa Uhuru wazindua miradi mbalimbali Mkoani Njombe
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amepokea mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Mji Makambako Mkoani Njombe leo tar 28 mei2018 ukiwa chini ya kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Charles Mwasambegu ukitokea mkoani Iringa na kulala katika viwanja vya polisi katika Halmashauri hiyo.
Mbio za mwenge huo ambao kauli mbiu yake ni ''ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA WEKEZA SASA KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU''Umefanikiwa kufungua miradi mbalimbali yenye thamani ya Bil 3,467elfu.
Kulingana na kauli mbiu ya Mwenge Serikali imeendelea kuhimiza wazazi au Walezi kuhakikisha wanatimiza wajibu kuwapeleka watoto wao Shuleni kwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano imeamua kutoa elimu bure pasipo na malipo. kuanzia Shule za Misingi hadi Kidato cha nne.
Imetumwa na mwandishi wetu Vintan Gadau
No comments
Post a Comment