Header Ads

Header ADS

CHADEMA Mkoa wa Mbeya wawavua madiwani wake watatu.

    Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoani Mbeya kimewavua  uanachama Madiwani watatu , ambapo uongozi wa Chama hicho umependekeza kuvuliwa uanachama wa madiwani hao watatu  wa chama hicho kutokana na kuonyesha utovu wa nidhamu .
















                     
                                                    Madiwani hao ni Geofrey Kanjigili wa Kata ya Sisimba , Newton  Mwatuboje wa Kata ya  Manga , Pamoja na  Hamphrey  Ngalawa  wa Kata ya Iwambi .Uongozi wa CHADEMA kupitia kwa Mwenyekiti  wake wa Jimbo la Mbeya Mjini  Obadia Mwaipalu  ametangaza uamzi huo leo Julai 21,2018 katika mkutano uliofanyika na Wanahabari  na kusema kuwa vikao halali vya Chama  vilivyofanyika  mara kadha kujadili  hatua stahiki ya Madiwani hao vimefikia uamuzi huo.
                   Pia amesemakuwa kutokana na utovu wa nidhamu kukiuka katiba ya Chama hicho  na kukaidi utekelezaji wa maazimio ya Uongozi  wamepeleka mapendekezo yao kwa uongozi wa Chama ngazi ya kanda ya Nyasa  ili hatua zichukuliwe.

No comments

Powered by Blogger.