Kigwangala atoa siku 45 waliovamia pari la akiba kuhama .
Waziri wa Mali asili na utalii DK. Hamiss Kigwangalla ametoa siku 45 kwa wananchi wanaoishi kinyume cha sheria ndani ya kinga [Buffer Zone] za Pori la akiba Kijereshi kuondoka kwa hiari yao wenyewe kabla ya kuanza oparesheni ya kuwaondoa kwa nguvu.
Maagizo hayo yametolewa na Dk . Kigwangala wakati akitembelea pori hilo katika Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu wakati ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za Mikoani kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi pamoja na kutatua changamoto zake.
Mbali na hayo Kigwangala ,ameshuhudia wananchi wa kiwa wanafanya shughuli mbalimbali pamoja na kuweka makazi katika maeneo ya uhifahdi wanyama pori na kusema kuwa sheria za uhifadhi wa wanyama pori haziruhusu vitendo hivyo ndani ya maeneo ya uhifadhi pamoja na kingo zake ambazo ni mita 500 kutoka kwenye mpaka halisi wa eneo la uhifadhi.
Pia amewataka wananchi ifikapo tarehe 31Augost mwaka huu wananchi wote wawe wameshondoka kwa hiari yao wenyewe pia Kigwangalla amewaambia viongozi wanaohusika kusimamia hifadhi hiyo kuwa '' muwatangazie na mpime eneo hili vizuri na muweke alama ili wajue ni wapi wanatakiwa kuondoka na ikifika 1Septemba kama watakuwa hawajaondoka basi mfanye oparesheni maalumu muwaondoe na msafishe kila kitu 'Ni lazima ifike mahali kila mmoja anaheshimu sheria za nchi "Alisema Kigwangalla"
Waziri wa Mali asili na utalii Dk .Kigwangalla ,amemtaka mmiliki wa Hotel ya Kitalii ya Kijereshi Tented Camp , kurudisha kwa Kamishena wa aridhi hati miliki ya kipande cha aridhi chenye ukubwa wa hekta 464 kilichopo ndani ya pori hilo kwa kuwa ni batili ndani ya siku tisini ambayo nisawa na miezi mitatu.
Pia ameendelea kusema kuwa pori hilo lilianzishwa mwaka1994 na wakati muwekezeji huyo anadai kumilikishwa eneo hilo mwaka 1995, Jambo ambalo haliwezekani mtu binafsi kupewa hati ya kumiliki eneo lililopo ndani ya eneo jingine tena hifadhi.
Waziri Kigwangalla akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Logolambogo katika Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu wakati akitembelea pori la akiba la Maswa kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake.

No comments
Post a Comment