Header Ads

Header ADS

Meneja wa Pori la akiba la Uwanda asimamishwa kazi

              Waziri wa Maliasili na utalii Dk . Hamiss Kigwangala  amemsimamisha kazi meneja wa Pori la Akiba la Uwanda ambalo lipochini ya usimamizi wa Mamlaka ya  Wanyama Pori  Tanzania [TAWA] Mark Chuwa kwa kushindwa kuondoa mifugo anina ya Ng'ombe 12,000 Pa moja na Wafugaji waliofamia pori hilo.





















     Itakumbukwa kuwa Pori hilo linapatikana Bonde la ziwa Rukwa  katika Wilaya ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa ,Kigwangala ,amemsimamisha kazi meneja huyo baada ya kusomewa taarifa ya Mkoa wa Rukwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk .Halfany  Haule akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa , Joachim  Wangoma .
           Hamisi Kigwangala ,ambaye ndiye mwenye dhamana ya maliasili na Utalii amesikika akisema kuwa ,,Umeshindwa kazi Chawa ,,kwa sababu una askari 26 na wewe mwenyewe lakini umeshindwa kuwaondoa ng'ombe na wafugaji waliovamia na kuchunga katika pori la akiba la Uwanda 'Lakini bado mnalipwa mshahara bila kutimiza wajibu wako ,ninatarifa ninataarifa kuwa mnapokea rusha"Kuanzia sasa nakusimamisha kazi na` nataka maelezo ya kutosha.
            Ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kikazi Dk .Kigwangala yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne ambayo ameanza Mkoa wa Rukwa.

No comments

Powered by Blogger.